Wageni wanaweza kufika kwenye kisiwa cha Bongoyo kwa boti au kivuko kutokea SlipWay shopping centre iliyopo Msasani Peninsula pwani ya Dar es Salaam. Kivuko kinaondoka kila baada ya masaa 2 kuanzia saa 3:30 asubuhi na kurudi Dar mwisho saa 11 jioni. Kivuko kinaenda kwa dakika 30 tu.