[Skip to Content]Privacy Policy
 
Dar es Salaam, Tanzania  | +255-222-162-333
 • Vyumba vya Ramada Resort Dar es Salaam
 • Vyumba vya Ramada Resort Dar es Salaam
 • Vyumba vya Ramada Resort Dar es Salaam
 • Vyumba vya Ramada Resort Dar es Salaam
Hifadhi

Ramada Resort Dar Es Salaam

Tulia mapumzikoni kwa kukaa katika malazi ya mbele ya fukwe yenye huduma zilizoundwa kwa ajili ya kurahisisha starehe yako. Samani za kisasa, matandiko ya vitanda ya kifahari ya sufi, na mavazi laini ya kuogea na malapa yakikukaribisha uvue viatu vyako na ukae kwa muda. Madirisha makubwa yanatoa mwanga wa kutosha wa asili na roshani binafsi ikijitokeza usawa wa bahari ya Hindi. Runinga bapa zenye matangazo ya hali ya juu zenye vin'gamuzi vya masafa ya mbali kukuburudisha wakati ukiwa hapa.
Chumba Kikubwa hapa Ramada Resort Dar es Salaam

Chumba Kikubwa

Jiweke katika starehe na fahari ndani ya vyumba vyetu vikubwa kabisa ambavyo vina vitanda vya hariri, na matandiko ya vitanda laini, mavazi ya kuogea na malapa, runinga bapa zenye matangazo ya vin'gamuzi vya masafa ya mbali, sehemu ndogo ya vinywaji, roshani binafsi, na inayojitokeza usawa wa bahari ya Hindi au katika bustani ya kupumzisha miguu yako.
Viwango vya kuanzia: $150
Chumba chenye hadhi ya Urais hapa Ramada Resort Dar es Salaam

Chumba cha Kipekee

Furahia mapumziko kamili katika chumba chetu cha kipekee chenye kitanda cha hariri cha kifahari, chenye uchaguzi wa kuunganishwa na mtandao, matandiko ya vitanda laini mavazi ya kuogea na malapa, runinga bapa zenye matangazo ya vin'gamuzi vya masafa ya mbali, sehemu ndogo ya vinywaji, baraza binafsi yenye chemchem, inayojitokeza usawa wa bahari ya Hindi.
Viwango vya kuanzia: $350
Chumba chenye hadhi ya Viongozi hapa Ramada Resort Dar es Salaam

Vyumba vyenye hadhi ya Viongozi

Wafanya biashara wasafiri wanaweza kupumzika baada ya siku za kazi au michezo katika vyumba vyetu vyenye hadhi ya Viongozi,yenye matandiko ya vitanda laini, mavazi ya kuogea na malapa, luninga bapa zenye matangazo ya vin'gamuzi vya masafa ya mbali, sehemu ndogo ya vinywaji, roshani binafsi , muonekano wa kusisimua usawa wa bahari ya Hindi.
Viwango vya kuanzia: $250
Hoteli ya Dar es Salaam - Vyumba ya kawaida

Vyumba vya Kawaida

Pumzika katika vyumba vyetu vya kawaida vyenye yenye matandiko ya kitanda laini mavazi ya kuogea na malapa, runinga bapa zenye matangazo ya vin'gamuzi vya masafa ya mbali, na sehemu ndogo ya vinywaji.
 

Huduma

 • Roshani binafsi
 • Bahari & vyumba vinavyotazama bustani
 • Runinga bapa
 • Matangazo ya Runinga ya vin'gamuzi vya masafa ya mbali
 • Sehemu ndogo ya vinywaji
 • Mashine ya kutengeneza Kahawa / chai
 • Pasi/ Meza ya kupigia pasi (Kunyoosha Nguo)
 • Mavazi ya kuogea & malapa
 • Bafu lenye bomba la mvua
 • Huduma unazohitaji kutumia bafuni hupatikana
 • Kifaa cha kukaushia nywele
 • Vyumba vyenye usalama
 
Agiza Sasa