facebook Privacy Policy [Skip to Content]Privacy Policy

 

Sehemu ya Mapumziko, Ramada Dar es Salaam Sera ya Faragha

Imani Zetu Msingi Kuhusiana na Faragha ya Mtumiaji Na Ulinzi wa Data

 • Faragha ya mtumiaji na ulinzi wa data ni haki za binadamu
 • Tuna wajibu wa kuwalindtunza watu ndani ya data yetu
 • Data ni wajibu, inapaswa kukusanywa tu inapohitajika kabisa
 • Tunachukia taka kama unavyochukia!
 • Hatutawahi kuuza, kukodisha wala kusambaza au kuweka maelezo yako ya binafsi hadharani

Sheria Muhimu

Pamoja na biashara yetu na na mifumo ya kompyuta ya ndani, tovuti hii imeundwa ili kutii sheria ya taifa na ya kimataifa kuhusiana na ulinzi wa data na faragha ya mtumiaji:
 

Maelezo ya Binafsi Kuwa Tovuti Hii Hukusanya Na Sababu ya Kuyakusanya

Tovuti hii hukusanya na kutumia maelezo ya binafsi kwa sababu zifuatazo:
 

Ufuatiliaji wa kutembelea tovuti

Kama tovuti nyingi, tovuti hii hutumia Google Analytics (GA) kufuatilia mawasiliano ya mtumiaji. Tunatumia data hii kutambua idadi ya watu wanaotumia tovuti yetu, ili kuelewa vyema jinsi wanavyopata na kutumia kurasa na kuona safari yao kupitia tovuti yetu.
 
Ingawa GA hurekodi data kama vile eneo lako la kijiografia, kifaa, kivinjari cha intaneti na mfumo wa uendeshaji, hamna kati ya maelezo haya yanayokutambulisha kwetu. GA pia hurekodi anwani ya IP ya kompyuta yako, ambayo inaweza kutumiwa kukutambua binafsi, lakini Google haitupi ufikiaji wake. Tunazingatia Google kuwa mchakataji mwingine wa data (tazama sehemu iliyo hapa chini).
 
GA hutumia vidakuzi, maelezo ambayo yanaweza kupatikana kwenye mwongozo wa wasanidi programu wa Google. Tovuti yetu hutumia utekelezaji wa analytics.js wa GA. Kulemaza kivinjari chako cha intaneti kutasimamisha GA kufuatilia sehemu yoyote unayotembelea kwenye kurasa ndani ya tovuti hii.
 
Kulemaza kivinjari chako cha intaneti kutasimamisha GA kufuatilia sehemu yoyoteyote unayotembelea kwenye kurasa ndani ya tovuti hii.
 
Mbali na Google Analytics, tovuti hii inaweza kukusanya maelezo (yaliyo katika kikoa cha umma) yanayohusiana na anwani ya IP ya kompyuta au kifaa kinachotumiwa kuyafikia.
 

Blogu

Endapo utaamua kuongeza maoni kwenye machapisho yoyote ambayo tumechapisha kwenye tovuti za blogu, jina na anwani ya barua pepe unayoweka vitahifadhiwa kwenye hifadhidata ya tovuti hii, pamoja na anwani ya IP ya kompyuta yako na wakati na tarehe ulipowasilisha maoni. Maelezo haya yanatumiwa tu kukutambua kama mchangiaji kwenye sehemu ya maoni ya chapisho husika la blogu na hayasambazwia kwa wachakataji wengine wa data walioorodheshwa hapa chini. Ni jina na anwani yako ya barua pepe pekee ulivyotoa vitakavyoonyeshwa kwenye tovuti ya umma.
 
Maoni yako na data ya binafsi inayohusiana nayo vitasalia kwenye tovuti hii hadi tuamue wakati unaofaa wa kuondoa
 
 • maoni au
 • kuondoa chapisho la blogu. Endapo utataka kufuta maoni na data ya binafsi inayohusiana nayo, tafadhali tutumie barua pepe hapa ukitumia anwani ya barua pepe uliyotumia kutoa maoni.
 
Ikiwa uko chini ya miaka 16 LAZIMA upate idhini ya mzazi kabla ya kuchapisha maoni kwenye blogu yetu.
 
DOKEZO: Unapaswa kuepuka kuweka maelezo ya binafsi yanayoweza kukutambulisha kwenye sehemu halisi ya maoni ya maoni yoyote ya chapisho la blogu unayowasilisha kwenye tovuti hii.
 

Fomu za mawasiliano na viungo vya barua pepe

Endapo utaamua kuwasiliana nasi ukitumia fomu ya mawasiliano kwenye ukurasa wetu wa Wasiliana nasi, hamna data unayotoa itahifadhiwa na tovuti hii wala kusambazwa kwa / kuchakatwa na wachakataji wengine wowote wa data waliobainishwa katikasehemu iliyo hapa chini. Badala yake data itachanganywa katika barua pepe na kutumwa kwetu kupitia Simple Mail Transfer Protocol (SMTP). Seva zetu za SMTP zinalindwa na TLS (wakati mwingine hujilakana kama SSL) kumaanisha kuwa maudhui ya barua pepe yanasimbwa kwa njia fiche kabla ya kutumwa kwenye intaneti. Kisha maudhui ya barua pepe yanasimbuliwa na kompyuta na vifaa vyetu vya ndani.
 

Jarida la barua pepe

Ukiamua kijiunga kwenye jarida letu la barua pepe, anwani ya barua pepe unayowasilisha kwetu itasambazwa kwa Benchmark wanaotupa huduma za utafutaji soko kwa barua pepe. Tunachukulia Benchmark kuwa mchakataji mwingine wa data (tazama sehemu iliyo hapa chini). Anwani ya barua pepe unayowasilisha haitahifadhiwa ndani ya hifadhidata ya tovuti hii wala katika mifumo yoyote ya kompyuta ya ndani.
 
Anwani yako ya barua pepe itasalia ndani ya hifadhidata ya Benchmark mradi tu tuetaendeleea kutumia huduma za Benchmark kwa ajili ya utafutaji soko kwa barua pepe au hadi uombe iondolewe kwenye orodha. Unaweza kufanya hivi kwa kujiondoa kwa kutumia viungo vya kujiondoa vilivyo katika majarida yoyote ya barua pepe tunayokutumia au kwa kuomba kuondoa kupitia barua pepe. Unapoomba kuondoa kupitia barua pepe, tafadhali tutumie barua barua pepe ukitumia anwani ya barua pepe ambayo imesajiliwa kwenye orodha ya barua.
 
Ikiwa uko chini ya miaka 16 LAZIMA upate idhini ya mzazi kabla ya kujiunga kwenye jarida la barua pepe.

Wachakataji Wengine wa Data

Sisi hutumia washirika wengine kuchakata data ya binafsi kwa niaba yetu. Washirika hawa wengine wamechaguliwa kwa uangalifu na wote wanazingatia sheria iliyowekwa katika sehemu iliyo hapo juu.
 
 
 

Sera ya Vidakuzi

Sera hii inaangazia matumizi ya vidakuzi na teknolojia nyingine. Aina za vidakuzi tunavyotumia viko katika kategoria 3:
 • Vidakuzi muhimu na teknolojia sawa

  Hivi ni muhimu kwa kuendesha huduma zetu kwenye tovuti na programu zetu. Bila matumizi ya vidakuzi hivi sehemu za tovuti zetu zisingefanya kazi. Kwa mfano, vidakuzi vya kipindi huruhusu hali ya uondokaji inayofanana na bora kwa kasi ya mtandao wa mtumiaji na chaguo la kifaa.
 • Vidakuzi vya Analytics na teknolojia sawa

  Hivi hukusanya maelezo kuhusu matumizi yako ya tovuti na programu na hutuwezesha kuboresha jinsi inavyofanya kazi. Kwa mfano, vidakuzi vya analytics hutuonyesha kurasa ambazo zinatembelewa sana. Pia husaidia kutambua matatizo yoyote uliyo nayo kufikia huduma zetu, ili tuweze kutatua matatizo yoyote. Mbali na hayo, vidakuzi hivi huturuhusu kuona mienendo ya jumla ya matumizi kwa kiwango cha jumla.
 • Vidakuzi vya kufuatilia, kutangaza na teknolojia sawa

  Sisi hutumia aina hizi za teknolojia kutoa matangazo ambayo yanafaa sana mambo yanayokuvutia. Hii inaweza kufanywa kwa kuwasilisha matangazo ya mtandaoni kulingana na shughuli za awali za kuvinjari tovuti. Vidakuzi huwekwa kwenye kivinjari ambacho kitakumbuka tovuti ulizotembelea. Kutangaza kulingana na kile ambacho umekuwa ukiangalia huonyeshwa kwako unapotembelea tovuti zinazotumia mitandao sawa ya kutangaza.
Pia tunaweza kutumia vidakuzi na teknolojia sawa kukupa matangazo kulingana na mahali ulipo, kukupa huduma ya kubofya na matumizi mengine sawa kwenye tovuti na programu zetu.
 

Ukiukaji wa Data

Tutaripoti ukiukaji wowote wa data usio wa halali wa hifadhidata ya tovuti hii au hifadhidata za wachakataji wetu wengine wowote kwa mtu yeyote na watu wote na mamlaka ndani ya saa 72 za ukiukaji ikiwa imedhihirika kuwa data ya binafsi iliyohifadhiwa katika njia inayotambulika imeibwa.
 

Mabadiliko Kwenye Sera Yetu Ya Faragha

Sera hii ya faragha inaweza kubadilika kila mara ili kutii sheria na/au maendeleo ya tasnia. Hatutawafahamisha wateja wetu au watumiaji wa tovuti kuhusu mabadiliko haya. Badala yake, tunapendekeza kuwa uangalie ukurasa huu mara mojamoja ikiwa kuna mabadiliko yoyote ya sera.
Kwa kuweka anwani sahihi ya barua pepe ambayo una idhini ya kufikia, tutakufahamisha maelezo yoyote ya binafsi tunayokusanya ambayo yanahusiana na anwani hiyo ya barua pepe na jinsi tunavyoyadhibiti.
 
 
whatsapp