facebook Restaurants in Dar Es Salaam - Ramada Resort by Wyndham Dar Es Salaam [Skip to Content]Privacy Policy
  • Vyakula ndani ya Ramada Resort Dar Es Salaam
  • Vyakula ndani ya Ramada Resort Dar Es Salaam
  • Vyakula ndani ya Ramada Resort Dar Es Salaam
Kwa maswali? Tupigie (Jumatatu - Ijumaa saa 3 - 11 jioni)
AU

Migahawa yenye hadhi ya Kimataifa jijini Dar Es Salaam

Dar es Salaam ni jiji la ladha na tamaduni, na migahawa ya kimataifa ambayo iko tayari kuvumbuliwa. Kula Ramada Resort kwenye migahawa na baa yenye handi ya kimataifa na menyu za kipekee za vyakula na vinywaji. Furahia chakula chako ukiwa umezungukwa na mandhari ya Bahari ya Hindi.
 
Furahia mapishi ya wataalamu wetu wakiwa wanatengeneza vyakula vyenye hadhi ya Kimataifa. Ladha halisi ya Kiafrika. Chochote unachopenda, utapata migahawa ya uhakika hapa ukiwa Dar es Salaam.

Ofa za migahawa

Vifurushi vya vifungua kinywa, Ramada Resort Dar Es Salaam
 

Bubbles & Brunch

Chakula cha mchana Jumapili ukifurahia ladha adimu! Lunch zetu ni pamoja na wine na menyu zinazokupa fleva asili na Kimataifa
Pizza karibu na bwawa la kuogelea, ramada Resort Dar Es Salaam
 

Jipumzishe pembeni ya swimming pool ukila Pizza

Una hamu na Pizza? Hii bahati yako… Ramada tunakupa menyu za pizza za aina mbalimbali. Tumeweka viungo kadha wa kadha na sosi tofauti kuzifanya
Msimu wa Soka ndani ya Ramada Resort
 

Msimu wa soka

Msimu wa soka umerudi. Njoo ushangilietimu yako kila wikiendi ukiwa Oceans 171 Bar at Ramada Resort Dar es Salaam(Ijumaa, Jumamosi na Jumapili. Njoo uangalie mechi live kwenye mandhari ya kimchezo ukifurahia na happy hour, menyu za kipekee na mengi zaidi. Tupigie simu kupitia +255-222-162-333 kuweka rizavu.
Keki na Ramada Resort Dar Es Salaam
 

KEKI

Sehemu pekee kwa ajili ya kila hafla/sherehe. Eneo limeandaliwa kwa ustadi kwa hafla mbalimbali kama bethidei, maharusi, mahafali, send off party, kipaimara na maadhimisho mengine. Piga simu namba +255-222-162-333 u tuandikie kupitia info@ramadaresortdar.com tukuandalie sherehe yako unavyostahili.
Jumamosi ya Mandhari na Ramada Resort
 

Mahadhi ya Jumamosi

Ramada Resort Dar inakuletea - usiku wa S.W.A.T. Furahia Jumamosi yako ukifurahia upishi a vyakula vya asili ya Waswahili na ladha ya tamu ya samaki wa baharini kila Jumamosi hapa Market Restaurant. Tupigie kwa simu +255-222-162-333 au tuandikie barua pepe kupitia info info@ramadaresortdar.com kufanya booking.
Mgahawa wa Living Lounge Ramada Resort Dar Es Salaam

Sehemu ya mapumziko

Jiachie na marafiki na familia ufurahie ladha ya chai tamu, menyu za kipekee kwenye mandhari yenye mwanga unaovutia ukiwa the Living Lounge jijini Dae es Salaam.
Soko ndani ya Ramada Resort Dar Es Salaam

Sokoni

Menyu zenye vyakula vye asili ya Kitanzania, na vya Kimataifa. Vyakula vinavyovutia vikiandaliwa papo hapo ukiona kwenye jiko la wazi Dar es Salaam kwenye mgahawa wa The Market.
Ramada Resort Africana Grill

Mapishi ya Kuchoma ya Africana

Mgahawa wenye aina tofauti za milo ya nyama, kuku na samaki maji chumvi . Furahia steki nono za nyama zikiandaliwa ukiona kwenye jiko la wazi unapoweka oda yako.
Ocean's 171 ndani ya Ramada Resort dar Es Salaam

Bahari171

Furahia kunywa na marafiki. Pata mivinyo na pombe za hadhi ya juu, vinywaji vikali, pamoja na apetaiza za uhakika.
 
List ya Vyakula
  • Migahawa mbalimbali ya Vyakula

  • Mivinyo ya kulipia

  • Viungo vya kienyeji

  • Sahani za kugawana

  • Sehemu binafsi za juu ya Hoteli

whatsapp