AIpo hapo tu nje ukitoka! Mchanga mweupe na bahari mwanana pembeni ya bwawa letu la kuogelea na njia nzuri iendayo sehemu kimya,tulivu na yenye amani ya Jangwani Beach.Muonekano mawingu na maji vuguvugu ya bahari hakika ni paradiso.
ANdio! Tunafanya. Tujulishe namba ya ndege yako, na tutakuwa Airport tukikusubiri.Umbali ni wa kilometa 28 ambao ni chini ya lisaa limoja tu tutakuwa tumekufikisha kwenye beach yako ya kujinafasi.
AKiukweli kuna jumla ya aina tano tofauti za mapishi. Chagua kuanzia mapishi mepesi,mapishi ya kawaida kwenye Living lounge, Vyakula vya vya mitaani vya hadhi ya kimataifa katika mgahawa wetu wa Sokoni, vyakula vya kitanzania na muonekano wa bahari katika Africana Grill, Tapas na mchanganyiko mbalimbali wa vinywaji katika Ocean's 171, na burudani nzuri juu kabisa ya Hoteli ikiwemo pizza za motomoto na vinywaji murua ndani ya Sky Beach Lounge.