Kisiwa cha Bongoyo: Fukwe na chakula
Panda kivuko bahari ya Hindi hadi kisiwa cha Bongoyo pwani ya Msasani Peninsula Dar es Salaam. Sehemu hii tulivu inafaa kwa safari ya kutwa kutoka Ramada Resort Dar es Salaam, ukifurahia siku yako kwenye fukwe zenye mchanga mwenpe na maji safi.
Panda boti kwa safari fupi na utapokelewa na kwa ukarimu na wenyeji walio tayari kukutembeza kisiwani. Kula samaki maji chumvi kama Changu na Kalamari kwenye mgahawa. Kisiwa cha Bongoyo ni sehemu sahihi ya mapumziko, kujituliza na kujiliwaza.
Maelezo
Bei -
Bei ya kivuko ni shilingi 35,000 (kama dola 20) kwa mtu mmoja. Shade banda inakodoshwa kwa shilingo 5,000 (dola 3) kila mmoja.Masaa -
Kivuko kinakwenda kisiwani kila siku kuanzia saa 3:30 asubuhi kila baada ya masaa 2 hadi saa 9:30 jioni. Kivuko cha mwisho inarudi kutoka kisiwani saa 11 jioni.Shughuli
- Boti
- Kuogelea
- Fukwe
- Kupiga mbizi
- Matembezi
- Chakula