Ramada Resort Dar Es Salaam
Tinga Tinga ni aina ya sanaa ya nyumbani inayojulikana kwa rangi zinazon'gaa, aina ya mapambo na viduara vidogo vidogo vinavyozunguka mchoro. Jina hili linatokana na Edward Saidi Tingatinga, msanii wa nyumbani alieanzisha mtindo huu, Tinga Tinga ni maarufu Tanzania nzima na duniani. Wageni wanaweza kununua Tinga Tinga katika njia mbalimbali, kutoka kwa wasanii wanaopamba kila kitu kutoka vitambaa ghali vya kuchorea mpaka vifaa vya udongo kwa michoro ya kipekee. Tinga Tinga asilia inaweza kupatikana kituo cha sanaa na ushirika kilichopo barabara ya Morogoro, Oyster Bay.Maelezo
Bei -
Bure.Saa -
Wazi kila siku kuanzia 2:00 asubuhi-12:00 jioni.Matukio -
NoneShughuli
- Wasanii wa kazi za Tinga Tinga
- Manunuzi