Fukwe ya Bluu
Muonekano wa bahari na wakati mzuri wa kufurahia ni moja ya orodha za Sky Beach,sehemu maalumu na binafsi ya juu kabisa ya hoteli ambapo upana wa bahari ya hindi huonekana vizuri. Unaweza kuandaa shughuli ya mkusanyiko wa watu mbalimbali au binafsi chini ya paa zuri lionyeshalo nyota na mawingu wakati wageni wakifurahia vinywaji mchanganyiko,mivinyo na bia.Au andaa mapishi binafsi pamoja na vitafuno vitamu kutoka kwa wapishi wetu maridadi.Kuanzia mikusanyiko binafsi mpaka sherehe kubwa za harusi, Sky Beach ni mahala sahihi kwa shughuli yako.